Thursday, 3 November 2016

Wasamaria walivyomfuta machozi Mwanafunzi wa UDSM aliyelia gazetini kwa kukosa mkopo

Alionekana kwenye Magazeti likiwemo la Mwananchi akitokwa machozi na kujifuta baada ya kuona jina lake halipo kwenye orodha ya waliopata mkopo chuo kikuu cha Dar es salaam, jina lake ni Edson Mwakyombe ambaye alifaulu Form VI kwa Dividion 1.8
Baada ya Wasamaria kumuona kwenye gazeti, kupitia kwa Mwanasheria Albert Msando wakaomba kukutana nae tayari wakiwa wameguswa kumsaidia malipo na wakafanikiwa kulitimiza hilo November 1 2016.
Kiufupi ni kwamba Wasamaria wawili Isaria Mlaki na Andrew Komba waliojitokeza kumsaidia wamemuahidi kumsomesha kwa miaka miwili kila mmoja akimsomesha kwa mwaka mmoja.
Baada ya hayo Edson mwenyewe amesema ‘Nashukuru kwamba jambo hili limewagusa watu, naiomba serikali matatizo kama haya ya mkopo wayaangalie sana kwani kuna baadhi ya watu pia wanateseka sana huku chuoni kwetu, pia ninawaahidi hawa waliojitokeza kuwa nitahakikisha nafanya vizuri katika masomo yangu
.
Edson Mwakyombe akiwa na msamaria wake Isaria Mlaki aliyejitolea kumsomesha mwaka wa pili chuoni
.
Andrew Komba ambae ambae amejitolea kumsomesha masomo yake ya mwaka wa kwanza, Edson katikati na Mwanasheria Albert Msando

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM