Monday, November 21, 2016

WANAUME WAANZA KUHASIWA KENYA...150 WAMEJIANDIKISHA KUKATWA MIRIJA YA UZAZI

Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka chumba cha upasuaji kutoka mjini Nairobi, Kenya kama njia ya kuhamasisha watu kuhusu njia hiyo ya kupanga uzazi .Takriban wanaume 150 walijiandisha kufanyiwa shughuli hiyo iliyochukua muda wa takriban dakika 20.Madaktari walifanya shughugli hiyo nyuma ya jukwaa lilifunikwa katik ukumbi wa sanaa mjini Nairobi.Wamaume nchini Kenya ambao mara nyingi wana hofu ya kufanyiwa zoezi hilo la kupanga uzazi mara nyingi uhofia kunyanyapaliwa..
Wale wanaoendesha kampeni ya zoeizi hilo wanasema kuwa ndiyo njia salama ya kupanga uzazi.
"Wanaume wengi hudhani kuwa zoezi hilo humnadili mwananamme kuwa mwanamke," Jack Zhang ambaye ni daktari kutoka Canada aliiambia BBC.
Baadhi ya wanaume wana hofu kuwa watu hufa kwa wingi barani Afrika kwa hivyo kuna haja ya kuzaa watoto wengi.Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, anasema kuwa baadhi ya wanaume walishiriki zoezi hilo baada ya kuchochewa na gharama ya kulea familia kubwa.
"Mbinu ambazo mke wangu alikuwa akitumia kupanga uzazi, zilikuwa na madhara kwake, kwa hivyo mimi niliamua kwenda kukatwa mirija ya ya uzazi," mwanamme moja aliiambia BBC.
Chanzo-BBC

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.