Friday, November 11, 2016

WANANCHI WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MANNE KONGOWE TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO MCHANA
Wananchi wakiangalia ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe, Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa.

Wananchi wakiangali basi dogo aina ya Coster ya abiria namba T 415 DCC ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa.


Wananchi wakiwa eneo la ajali

Wananchi wakiwa eneo la ajali.

Ofisa wa Jeshi la Polisi akiwa eneo la ajali akichukua taarifa.

Prado yenye namba T 177 AHH iliyohusika katika ajali hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATU kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.Ajali hiyo ilitokea saa sita mchana na kuhusisha magari hayo lori la mafuta aina ya Scania lenye namba T 617 AQQ, Coster ya abiria namba T 415 DCC inayofanya safari zake kati ya Kilwa Masoko na Mbagala, Prado yenye namba T 177 AHH, pikipiki na lori jingine.
Ofisa wa Polisi aliyekuwepo eneo la ajali ambaye alitambulika kwa jina moja la Emanuel alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
"Nimefika sasa hivi bado hatujajua chanzo cha ajali wala watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa" alisema ofisa huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alipopigiwa simu ili kuthibitisha ajali hiyo alikiri kutokea hata hivyo alisema alikuwa hajapata taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Wilaya hiyo ambaye alikuwepo eneo la tukio.Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke kwa matibabu.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.