Friday, 4 November 2016

WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO MOROGORO WAFUNGA BARABARA


Wafanyabiashara wadogowadogo wengi wao wakiwa mama lishe pamoja na wauza matunda na mbogamboga katika manispaa ya Morogoro wamefunga barabara na kuchoma moto katikati ya soko kuu wakipinga hatua ya mgambo wa manispaa kumwaga na kuwanyang’anya biashara zao.
Wakizungumza kwa masikitiko wafanyabiashara hao wadogo wametupia lawama uongozi wa manispaa kushindwa kuwaonyesha eneo maalumu la kufanyia biashara na kuwaacha wakitangatanga huku wakikabiliwa na mikopo mikubwa kwenye taasisi za fedha.
Kufuatia vurugu hizo imemlazimu mkuu wa wilaya hiyo Bi, Regina Chonjo kufika katika eneo la soko kuu la manispaa ya Morogoro ambako ndiko wafanyabiashara hao wamefunga barabara na kuhitaji kufanya mazungumza baina yao na uongozi wa manispaa.
Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Morogoro Bwana Pascal Kihanga amesema kufuatia wafanyabiashara hao kutangatanga mjini manispaa inaandaa eneo maalumu kwa ajili yao.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM