Monday, 7 November 2016

Viongozi, wasanii pamoja na wadau wamlilia Samweli Sitta

Viongozi, wasanii pamoja na wadau mbali mbali nchini wamlilia aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samweli Sitta aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.
1-1
Viongozi hao pamoja na wadau wameandika ujumbe mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuonyesha kuwa taifa limepoteza mtu muhimu.

Makonda

Asante baba umenifundisha uongozi,Siku zote umeniambia nianze na mambo magumu kwanza ndiyo nifanye mambo mepesi,niwe na ngozi ngumu na wala nisikate tamaa. Hukuacha kuniombea na kunitia moyo hata wakati unaumwa, hakika wewe ni mwalimu ambae alama zako hazitafutika kamwe maishani mwangu.

Umenisomesha na hata kuniozesha, niseme nini ili dunia ielewe kuwa kwangu ulikuwa zawadi kutoka kwa Mungu,unyenyekevu,upole, na ujasiri wako ni dira tosha ya kuwatumikia Watanzania ambao mpaka sasa nina uhakika unawaombea. Nenda Mzee Sitta acha niendeleze viwango na kasi kwani ndiyo urithi ulioniachia.
Mwigulu Nchemba
Umenifundisha,umeniongoza kwenye siasa na kazi za serikali.Hakika tumepoteza mzazi,mlezi na kiongozi wa mfano.Pumzika kwa amani Mzee wetu Samwel Sitta.

Mrisho Mpoto
Pumzika kwa Amani baba yangu mzee Sita mbele yako nyuma yetu, pole nyingi kwa familia yote ya mzee #Sita pole Rafiki yangu @paulmakonda najua msiba Mkubwa sana kwako.
Mohamed Dewji
Pumzika kwa amani Mzee Samuel Sitta. Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi. Tutakukumbuka kwa upendo na uzalendo kwa wananchi wote wa Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF)Mwakifamba Simon
“Rest in peace samwel sitta umeondoka kimwili kifikra bado unaishi nasi kwa busara na hekima ulizokuwa umejaaliwa.

Shamsa Ford
‘Mungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi baba yetu.

Diamond Platnumz
“May God Rest your Loyal and Humble Soul in Peace,”

BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM