Thursday, 10 November 2016

Tuzo ya MTV EMA aliyoshinda Wizkid ilitolewa kimakosa, anapewa Alikiba

 
 MTV Europe music Awards 2016 ilifanyika weekend iliyopita ambapo Mtanzania mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alikua akiwania tuzo ya BEST AFRICAN ACT ambayo ilitangazwa siku ya tukio mshindi ni Mnigeria Wizkid.
Pamoja na kwamba Wizkid alitangazwa mshindi, mtandaoni ilikua inaonyesha Alikiba ndio anaongoza kwa kupigiwa kura na hapo watu wakaanza kuuliza kwa nguvu imekuaje? hata hivyo kulionekana mabadiliko baadae kwa rekodi hizo kutoonekana mtandaoni baada ya muda kupita.

 aarifa za uhakika kutoka kwenye Management ya Alikiba Exclusive kwa millardayo.com ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba.
Inaonekana Wizkid amefikiwa na taarifa na tayari post yake ya ushindi wa tuzo hiyo ameifuta kwenye mtandao wake, endelea kukaa karibu na millardayo.com na AyoTV ili kila kinachonifikia nikufikishie, usisahau ku-SUBSCRIBE youtube channel ya millardayo ili kupata matukio yote ya Tanzania kuanzia kwenye burudani, siasa, michezo na mengine.
Pia kaa karibu na page zenye jina la millardayo Twitter Facebook Instagram Snapchat APP kwenye Android na iOS kwa jina hilohilo la @millardayo ili kujiweka kwenye nafasi ya kupata notification ya kila habari inayonifikia.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM