
Idadi ya watu
waliyofariki kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini
mwa India, imeongezeka hadi tisini na tisa na kuwajeruhi mamia ya
wengine.
Treni hiyo ilikuwa
ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka
katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa
Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh
Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.
Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment