Tuesday, November 22, 2016

TOFAUTI NA NDONDI HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA FRANCIS CHEKANa Lewis Mbonde
TOFAUTI NA NDONDI HIKI NDICHO NNACHOKIFANYA "TAKA NI MALI KWA FAIDA YA TAIFA" Mimi ndio mwanamazingira namba 1 ktk manispaa ya morogoro na ni mtu wa kwanza kujitosa katika ukusanyaji wa chupa za plastiki ni mimi kupitia vijana wang niliowaajiri.Nilijifunza taka kupitia Teca,Modege,manispaa ya kinondoni na manispaa ya ilala nikiwa mzoaji taka kwenye magari.
Zamani chupa za plastiki baada ya kilichomo ndani yake kutumiwa, zilikuwa ama zikitupwa jalalani au kando ya barabara. Wakati mwingine ziliachwa ovyo kila kona, hivyo kuwa ni sehemu ya uchafu.Chupa tupu za maji nnazokusanya mitaani kwa mwezi ni zaidi ya kilo 5000 hadi 7,000 na mara baada ya kuzikusanya, nazisafirisha kwa magari ya kukodi hadi Dar es Salaam ili kuwauzia wafanyabiashara wachina,wahindi,watailand na wapakistan.Maafisa afya waanze kuwaelimisha vijana kwenye mashule na jamii kwa ujumla kuwa taka ni mali kupitia taka tunaweza kupata marigafi ya nguo,maligafi ya pikipiki,zinatoa ajira kwa vijana na kujiongezea kipato na nimewafunza vijana zaidi ya 50. Zamani chupa za plastiki zilikuwa ni kero, kutokana na kuzagaa ovyo, lakini sasa ni nadra kuzikuta mitaani chupa za plastiki zikizagaa ovyo hapa morogoro.Nilikusanya taka mpaka nikaandaa mechi yangu ya ubingwa wa Taifa mimi mwenyewe. Alisema Francis Cheka

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.