Monday, November 14, 2016

TB JOSHUA AFUNGUKA BAADA YA KUTOA UTABIRI WA UONGO KUHUSU HILARY CLINTON KUSHINDA URAIS MAREKANI

Mhubiri mashuhuri raia wa Nigeria TB Joshua amevunja kimya baada ya utabiri wake kuwa mgombea urais nchini Marekani Hillary Clinton angeshinda, kugonga mwamba.
Mhubiri huyo alikejeliwa kwenye mitandao ya kijamii wakati ujumbe wa utabiri wake, kufutwa na baadaye kurejeshwa katika akaunti yake ya Facebook kufuatia ushindi wa Donald Trump.
Hata hivyo, wafuasia wake wamekuwa wakimtetea wakisema kuwa utabiri wake ulitimia kwa sababu Bi Clinton alishinda wingi wa kura licha ya yeye kushindwa kutokana mfumo unaotumiwa kwenye uchaguzi nchini Marekani unaofahamika kama "electoral College".
Ujumbe mpya katika akaunti ya Joshua ya Facebook unaunga mkono maoni hayo,ukisema:
"Tumeona matokeo ya uchaguzi nchini Marekani. Baada ya kusoma, utaelewa kuwa hii inahusu kura nyingi, kura ya waamerika wengi"
"Kwa hali hii tunahitaji roho ya nabii kutambua au kumuelewa nabii." TB Joshua anaendelea kusema.tb-joshua-6655
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.