Saturday, 12 November 2016

Shilole ampongeza mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda kwa kufunga ndoa

bmrfsdehizp
Nuh Mziwanda, ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Flava aliyepata umaarufu wake kupitia sanaa ya muziki, akiwa na vibao vyake mahiri vilitokea kupendwa na wengi kama vile ‘Jike Shupavu’ na nyingine nyingi. Ambaye pia umaarufu wake ulizidi zaidi baada ya kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Msanii mwenzie Shilole a.k.a Shishi Baby baada ya kuonyesha mapenzi yake kwa Shilole kwa kujichora tatoo yenye jina lake.
Ni hivi karibuni tu waliachana kwa Nuh kukubali kwamba yeye na Shilole hawataweza kuishi wote kwani kulikua kuna fununu za kusema kwamba Shilole hakua anamuheshimu Nuh. Mungu si athumani wanasema waswahili, Nuh katika siku ya jana amefunga ndoa na msichana aliyekuwa akionekana nae sana baada ya yeye kuachana na Shilole. Jina lake linalofahamika sana ni lile analojiiita katika ukurasa wake wa Instagram Queen Nawal ambaye mpaka jana tayari alikua akijiita Mrs Mziwanda.
Picha za harusi yao:-
bmrfsdehizp
mziwanda
bmoaehygywy
Shilole yeye kwa upande mwingine alishasema hana tatizo na Nuh, na akatoa pongezi kufuatia hatua hiyo aliyoifanya Nuh Mziwanda:-

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM