Saturday, 5 November 2016

Serikali yaanza kutoa ajira kwa watumishi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema Serikali imeanza kuajiri watumishi wapya tayari imetoa nafasi 100 kwa hospitali mpya ya kisasa ya Mloganzila, iliyopo Dar es Salaam.
magu1-1
Akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu jijini Dar es salaam,Rais Magufuli alielezea suala hilo wakati akijibu swali na Anna Kwambaza wa TBC.
“Ajira sasa zinaendelea, tumetoa nafasi 100 kwa hopitali ya Mloganzila na zingine 200 zitafuata hivi karibuni. Hospitali hii itafunguliwa mwezi ujao” alisema Rais Magufuli.
“Serikali iliposimamisha ajira, haina maana kwamba ajira hazitakuwepo, bali ilikuwa inakamilisha kwanza kuhakiki wafanyakazi na kubaini wafanyakazi hewa,kazi ya kuhakiki watumishi hewa inaendelea na hadi sasa watumishi hewa 17,000 wameondolewa.”
“Isingewezekana kwa serikali kuendesha kazi ya kuhakiki watumishi na wakati huo huo kuajiri watumishi wapya, watumishi hewa wameleta madhara makubwa,”aliongeza.
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM