Monday, 28 November 2016

Rufaa ya Godbless Lema Yagonga Mwamba Leo Tena...Arudishwa Selo Rufaa ya Godbless Lema Yagonga Mwamba Leo Tena...Arudishwa Selo

Rufaa ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema iliyopangwa kutolewa leo imeshindikana baada upande wa Jamhuri kuweka pingamizi ya kuwasilisha notisi badala ya rufaa, ambapo Mbunge huyo amerudishwa rumande kwa mara nne.
Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu ambaye amesema wamefanya hivyo ili kuharakisha na wamekubaliana na pande zote mbili.

Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wameshakamilisha taratibu za kisheria kuhusiana na pingamizi hilo na wanasubiri pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.

Jaji aliyekuwa akisikiliza pingamizi hilo Fatma Masengi ameelekeza upande wa serikali wawasilishe hoja zao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.
TAZAMA:NIMEKUWEKEA VIDEO MSANII WA BONGO MUVI DR CHENI ADAI HAJAWAHI KUCHEPUKA NJE YA NDOA

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM