Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Ridhiwan Kikwete amesema urafiki kati ya baba yake na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa bado upo na wanawasiliana kwenye simu mara kwa mara.
Akiongea kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm mapema leo asubuhi, Ridhiwan amedai kuna watu ambao kazi yao ni ‘Kupika’ habari ndio wanaopotosha umma lakini mahusiano ni mazuri kati ya viongozi hao wastaafu.
“Lowassa na Kikwete ni Marafiki mpaka Kesho wanasalimiana, kumekuwa na upishi tu wa Habari, ukweli ni kwamba mambo ni mazuri” Alisema.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amekanusha uvumi unaoenea mitaani kwamba yeye ni tajiri na anamiliki mali nyingi nchini.
“Mimi ni tajiri wa Marafiki sio mali, ni porojo tu ninachomiliki kinanitosha mimi na ndugu zangu, sina Maghorofa wala vituo vya mafuta” Alimaliza Mh Kikwete