Saturday, 12 November 2016

PICHA:MAHARUSI WAFUNGA HARUSI WAKIWA KWENYE JENEZA.JIONEE MWENYEWE

Maharusi wengi hutamani siku ya harusi kuwa siku ya kitofauti zaidi katika maisha yao wakiamini ndio siku pekee ambayo ni ya furaha zaidi huku wengine wakitumia kila aina ya njia kuhakikisha sherehe yao inapendeza.
Utakuta wengine wanatumia usafiri wa farasi au magari ya kifahari kuhakikisha tu sherehe inakuwa ya kipekee zaidi kwao lakini kwa Jenny Buckleff ilikua tofauti kwani yeye alitumia jeneza kama usafiri wake.
Jenny alitaka kuwashangaza wageni waliofika kwenye sherehe yake hata kwa mumewe pia kwani hakumwambia mtu yoyote kuhusu uamuzi wake huo.
Siku ya sherehe aliingia ukumbini akiwa ndani ya jeneza lililokuwa likisikumwa kwa pikipiki huku kila mmoja akishikwa na butwaa kutokana na kitendo hicho ambacho si rahisi kutokea.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM