Sunday, November 20, 2016

Papa Francis awateua makadinali wapya 17

Kadinali Dieudonne Nzapalainga, kutoka Bangui ,Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kati ya walioteuliwa.

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis amewateua makadinali wapya wa kanisa katoliki kote duniani, wengi ambao wanashiriki katika kumchagua mrithi wake.

Makadinali hao wapya wanatoka mabara matano akiwemo mjumbe wa Vatican nchini Syria.

Sasa Papa Francis amechagua theluthi moja wa makadinali ambao watamchagua mrithi wake.

Ni makadinali walio chini ya miaka 80 tu ambao wanaweza kumchagua Papa mpya. 13 kati ya wale walioteuliwa wako chini ya miaka 80 na sasa wanahitimu kumrithi.Anthony Soter Fernandez kutoka Kuala Lumpur, apongezwa baada ya kuteuliwa kuwa kadinali

Ni mara ya tatua katika kipindi cha miaka mitatu ambapo Papa Franciss, ambaye ni Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini kuwateua makadinali wapya

Makadilani hao wapya wanatoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati , Bangladesh, Papua New Guinea na Mauriotius miongoni mwa nchi zingine.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.