Saturday, November 19, 2016

Mwanaume akiwa na sifa hizi 10 huwa na mvuto zaidi kwa wanawake

 7-ways-to-let-him-know-your-interested-3
Kama wewe ni mwanaume na una sifa hizi, basi fahamu kuwa sayansi imethibitisha kuwa una mvuto kwa wanawake

1. Sura Nzuri
Muonekano mzuri kwa mwanaume huwa ni kigezo cha kwanza katika maamuzi ya mwanzo kwa mwanamke lakini hata hivyo huwa ni katika mapenzi ya muda mfupi tu zaidi ya yale yanayodumu.
2. Ucheshi
Ucheshi kwa mwanaume si muhimu tu kama wenyewe bali humfanya mwanaume aonekane mwenye akili

3. Mwanaume anayetoa msaada

Wanawake hupenda wanaume wanaotoa msaada, wasio wachoyo pale wanapotafuta uhusiano wa muda mrefu

4. Utajiri/Uwezo wa kifedha

Ile imani kuwa wanaume wenye uwezo wana mvuto zaidi kwa wanawake ni kweli. Utafiti ulionesha kuwa wanawake huona wanaume wanavutia zaidi pale wanaposimama tu kwenye magari ya kifahari au nyumba, hata kama vikiwa sio vyao.
5. Umri Mkubwa
Wanawake hupenda wanaume wenye umri mkubwa kwasababu mara zote huamini kuwa wamekusanya vitu vingi na uzoefu katika maisha.
6. Ndevu
Ndevu zimekuwa zikichukuliwa kama zinazokera na kuvutia kwa wakati mmoja – yote hutegemea na mapenzi ya mtu.
7. Wagumu
Wakati utafiti wa zamani unasema kuwa wanawake huvutiwa na wanaume wanawaopenda, tafiti mpya zimedai kuwa kujifanya mgumu, kutojali kunawavutia wanawake. Kifupi, wanaweza kutaka kile wanachodhani hawawezi kupata.
8. Tafiti zinaonesha pia kuwa wanaume wenye mbwa huwavutia wanawake. Duh!
9. Wanawake kwenye tamaduni zote wameonesha kuvutiwa na wanaume wanaovaa rangi nyekundu
10. Wanawake wamethibitishwa pia kuwapenda wanaume majasiri na wasiogopa

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.