Saturday, 5 November 2016

Mwanamke Alala Kwenye Jeneza Siku Nzima ili Kupata Uzoefu wa Kifo

Imetokea Brazil na Mwanamke mwenyewe anaitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kulala kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza.

Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.
Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.

Ndugu zake walipingana sana na wazo lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho.

Mmiliki wa eneo la kuzikia liitwalo Eternal Garden Funeral home, Paulo Araujo, aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote, kama mgeni maalumu. Wakati akiwa ndani ya Jeneza mwanamke huyo alikua akifumbua macho na kufumba kama vile mtu aliyekufa na kufufuka.

Mwanamke huyo amesema alikuwa na ndoto ya kulala kwenye Jeneza tangu miaka 14 iliyopita na hakuwa akifikiri ingekuja kutokea akaitimiza, kwasasa amefurahi kutimiza alichokitaka kabla hajafa.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM