Tuesday, 22 November 2016

MKE WA DONALD TRUMP PAMOJA NA MTOTO WAO HAWATAISHI IKULU YA WHITE HOUSE,SABABU IKIWA NI HII.

Donald Trump ameelezea kuwa mke wake Melania Trump pamoja na mwanae Barron Trump,hawataweza kwenda kuishi nae kwa sasa katika ikulu ya Marekani White house,mara atakapotawazwa kuwa rais wa Marekani hapo mwezi January.Donald Trump atavunja mila na desturi za nchi ya Marekani ya kwamba mke wa rais "First lady" wa nchi ya Marekani lazima aishi katika ofisi ya rais.Lakini yeye aliweza kuzima uvumi uliokuwa unaenea kwa kasi mtandaoni na kusema kuwa mke wake pamoja na mtoto wake hataweza kuishi nae katika ikulu ya nchi ya Marekani,na atabaki katika jiji la New York mpaka majira ya kiangazi.
Na sababu yenyewe ya kwa nini mke wake pamoja na mtoto wao mwenye umri wa miaka 10 kubakia katika jiji la New York,ni kwa ajili ya mwanao kumalizia masomo yake katika shule moja ya private iliyoko katika jiji la New York.Chanzo cha karibu kabisa na bwana Trump kililiambia gazeti la New York post kwamba"Melania yuko karibu sana na mwanae Barron na wamekuwa na ukaribu sana hasa wakati wa uchaguzi"."Kampeni za uchaguzi wa Marekani imekuwa ngumu sana na imemuwia vigumu sana kwake kwa sababu ya mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea mitandaoni hasa kuonekana kwa picha za utupu za mama ayake mtandaoni,kumemchanganya sana".Alisema
Hata hivyo uamuzi wao wa kubaki katika nyumba ya bwana Trump utaongeza changamoto nyingi sana za kiulinzi,katika mamlaka ya ulinzi ya siri ya Marekani(secret service) na kitengo cha polisi(Police departiment),kwa sababu nyumba ya bwana Trump iko katika maeneo ya ubize mwingi sana.Na wanachama wa mtaa huo wanaweza kuingia katika jengo hilo na kutoka kama wanavyotaka.Ikumbukwe kwamba jengo hilo lilizungukwa na wapingaji wa matokeo pamoja na wanahabari wakiwemo polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM