Sunday, November 6, 2016

Meneja wa kundi la Yamoto Band, Said Fella akanusha taarifa zinazo dai kuwa yeye ndie amechangia kuua kundi la Jahazi Modern Taarab

Meneja wa kundi la Yamoto Band, Said Fella amefunguka na kusema yeye si sababu ya kuvunjika kwa Band ya Jahazi Modern Taarab ambayo ilikuwa inamilikiwa na Mzee Yusuph
baada ya wasanii wakongwe na nguli wa band hiyo kukimbilia kwenye Band mpya iliyoanzishwa na Said Fella.
Akizungumza kwenye eNEWZ Said Fella amedai kuwa yeye hajaivunja Jahazi bali wasanii hao wamekuja kwenye Band yake kwa lengo la kutafuta maisha na kufanya kazi ili watoto waweze kwenda shule.
"Mimi sijaivunja JAHAZI wale wamekuja na mimi nikasema sawa twendeni sababu mwisho wa siku wenyewe wanasema sisi tunapiga magitaa watoto wetu wasome na sisi tupate maisha, kwa hiyo la msingi na wewe unaweza kupata muda ukawatafuta wakina Mauji, Chid Boy, Bobu Ally, na wengine ukawauliza mbona mmefanya hivi wao watawambieni maana hayo ya kwako wao. Ila mimi najua Jahazi litaendelea kuwepo sababu ile ni Band kubwa na hawa kama wameamua kwenda kujitafutia basi sawa" alisema Said Fella
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.