Sunday, November 27, 2016

Makonda adai kuna watumishi wanatembea hirizi ili wasitumbuliwe

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake katika wilaya Kinondoni ambapo asubuhi ya leo amezungumza watumishi wa wilaya hiyo pamoja na kutoa baadhi ya maagizo.
4k0a7959
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kinondoni.
Akiongea na watumishi wa wilaya hiyo, Makonda amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii huku akidai kuna baadhi ya watumishi wanashinda kwa waganga wakienyeji ili wasitumbuliwe.
“Kuna baadhi ya watumishi wanatembea na hirizi ili wasitumbuliwe, wakikutana na viongozi wao wanazibinya,” alisema Makonda. “Mimi ninachokitaka kutoka kwenu ni kuwatumikia wananchi wa chini,”
Pia Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kupeleka malalamiko yao mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.
Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.
4k0a7920
Watumishi wa manispaa ya Kinondoni wakisikiliza jambo kwa makini
4k0a7923
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi (kulia) akimkabidhi taarifa mkuu wa mkoa wa Da es salaam, Paul Makonda

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.