Thursday, 10 November 2016

MAAJABU YA VIFO VYA MASWAHIBA WAWILI SITTA NA MUNGAI WENYE HISTORIA INAYOFANANA SOMA KUJUA ZAIDI. 
Na Sosy
SAMWEL Sitta ( 74) na Joseph Mungai ( 73) uswahiba wao ilianza tangu shule ya sekondari ya Tabora Boys. Maswahiba hawa waliopishana mwaka mmoja tu  moja na watazikwa siku moja wanahistoria yenye kufanana.

Wawili hawa wamefariki ndani ya juma moja (wiki ) na kupishana siku moja tu.
Historia ya maisha ya maswahiba hawa ni wawili ambao wote upande wa mama zao wametokea kwenye koo za kubwa za mafichu hapa nchini.
Mama wa marehemu Sitta, Zuena Said Fundikira, ni biinti wa Chifu Fundikira ambaye babu yake ni Mtemi Isike Kiyungi.
Mama wa marehemu  Mungai anatokana na ukoo wa Malangalila unatokana na Chifu Mkwawa. Hivyo, akina Malangalila na Mwamuyinga ni wajomba zake Joseph Mungai kutoka ukoo wa Kichifu wa Mkwawa.
Wawili hawa mbali ya uswahiba wao wa tangu shule uliowapelekea hadi kufanya kazi kama Mawaziri kwenye Serikali za Awamu Nne.
Ni watani wa jadi. Ni kwa vile Wahehe chini ya Chifu Mkwawa walipigana na Wanyamwezi chini ya Mtemi Isike .
Katika namna ya kusuluhisha mgogoro, Chifu Isike alimuozesha binti yake kwa Chifu Mkwawa. Kikosi kidogo cha Wakonongo kilitumwa na Isike kumsindikiza binti huyo. Walipoikaribia Iringa, Mkwawa alituma watu wake kwenda kumpokea binti huyo nje kidogo ya Iringa mahali ambapo hadi hii leo panaitwa Ikonongo.
Na Wakonongo wale waliamua kuweka makazi yao hapo. Ni nje kidogo ya Manispaa ya Iringa, na dalili za ujio wa Wakonongo hapo ni uwepo , hadi leo, wa watu wa asili ya Kikonongo na miti mingi ya miembe waliokuja nao Wakonongo kutoka Tabora, enzi hizo.
Ni simanzi kwa maswahiba hawa kutuagana Chifu Mungai ameagwa leo, na mwenzake Chifu Sitta ataagwa kesho. Wote wawili watazikwa katika siku moja ya Jumamosi, mmoja Mufindi na mwingine Urambo.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM