Sunday, 20 November 2016

Kukamatwa kwa kinara wa matusi Instagram kuwe funzo kwa wengine wanaochezea sharubu za sheria ya makosa ya mtandao

https://3.bp.blogspot.com/-QVM9and4X24/WC60ibuDRWI/AAAAAAABQyA/7G20AZJTLp4RW0HJNW2ibkcG_4vcFfuYwCLcB/s640/sk.jpg

“Mwanangu unafanya nini chumbani,” ni kauli ya mama kwa mwanae aliyejifungia chumbani kwake akiwa busy utadhani anaandika proposal ya biashara ya mabilioni.

“Ninaupdate kitu kwenye Instagram mama,” anajibu kijana huyo ambaye kutwa nzima simu yake haichomoki mkononi mwake. Mama yake anapata matumaini kuwa, baada ya mwanae kumaliza kidato cha nne, ameamua kutumia simu kujifunza mengi ya dunia na si mtu wa kuzurura tena. Hiyo inakuwa furaha kwa mamaye anayejiaminisha kuwa kazaa jembe! Laiti kama angejua anachokifanya mwanae kutwa nzima, angelizimia na kulazwa hospitali kwa presha.

Kumbe mwanae ni kinara wa matusi Instagram. Anatumia jina feki na kile kinachompa ubusy, ni kuandika mikeka ya matusi kwa mastaa wa Kibongo. Kwake hiyo ni kama kazi, na amejipatia mashabiki wengi.

Akaunti za aina hii zipo nyingi na zinatukana watu kama zinalipwa mshahara. Mmoja amekamatwa wiki hii na sasa anajuta kuzichezea sharubu za sheria za makosa mtandao.

Akaunti ya @shilolekiuno_official ninaifahamu kwa muda na imekuwa ikinifollow pia. Akaunti hii ni miongoni mwa zile zilizobobea kwa kutukana mastaa.

Kwakuwa wanaomiliki akaunti hii hujificha kwenye kivuli cha akaunti bandia, ni ngumu kujua wahusika. Na pindi wanapokamatwa, ndio unakuja kushangaa kumbe ni bwana mdogo kama huyo niliyemuelezea hapo juu. Anatia huruma.

Akaunti hii ilikuwa imezidi kwa matusi – na ilikuwa ikitema matusi ya nguvu kweli, matusi mazito. Hii ni post ambayo huenda ndiyo ilimponza na kujikuta akinaswa na chupi mkononi:

NYIE MSNUNUE HIYO PERFYUM NIYA KIS*NGE SANA,, PERFYUM IMETENGEBEZWA KWA MAJI YA MAITI ILI KILA MTU ATAKAE JIPULIZIA ANAKUA MSUKULE WAKE WA KWENYE SHOW 😎KWANZA HIYO PERFYUM HAINA UBORA WOWOTE ULE 😈PERFYUM IMETENGENEZWA KWA MKOJO WA BI SANDRA, PERFYUM IMECHANGANYWA KWA JASHO LA MATAK*N YA #BABUTALE NA #SALLAM_SK, PERFYUM IMEWEKEWA KAHARUFU ZA MAKWAPA YA HARMONIZE NA RAYNAVY 😩PERFYUM IMECHANGANYWA NA MIUDENDA YA TIFA πŸ˜₯PERFYUM FAKE PERFYUM IMECHANGANYWA NA MAKOOZI YA #HALIMAKIMWANA 😏PERFYUM IMECHANGANYWA NA UARISHO WA #QNDARLIN 😭PERFYUM IMECHANGANYWA HARUFU YA MDOMO YA MKUNA MAV*Z ZARITHEBOSSLADY PERFYUM FAKE JAMANI PERFYUM IMECHANGANYWA NA UTEUTE WA K*MAMAN WA #ESMAPLATNUMZ JAMAN NAWAAMBIEN HAYO MAPERFUM YA KICHAWI YATADOROLA HAYATONUNULIWA KAMA YALE MALIPSTICS YA WEMA MALIPSICS YA WEMA SEPETU SASA HIVI MABEKITATU WAKE NYUMBU WAPO WANAYACHEZEA MSITA
πŸ˜‚NYIE MASHABIKI WAFI**AJI WA #WCB HUYO SHOGA WENU #SUPERNYAMWERA ANAWIVU KISIM CHA MAMA YAKE KIMEMSIMAMA KAMA MVUKE WA UJI 😎YAAN KILA KITU ANAFANYA ILI AMJIBU #KINGKIBA UJUE KINGKIBA ALIIMBA KIFARANSA KWENYE NYIMBO YA AJE YY CHAIJABAA ETI AKAMJIBU KWA KUIMBA KIHAYA KWENYE #SALOME KINGKIBA KAONESHA GHOROFA YAKE YEYE CHAIJABAA AKAONESHA KACHUMBA KAKE KA KUPANGA SOUTH 😈KINGKIBA ALIONESHA KIFUA STEJINI #CHAIJABAA AKAONESHA MK*NDU STEJIN DUUUHπŸ˜₯ UYO MK*NDU πŸ‘†#DOMO ALITOA MATISHIRT YAKE YA WCB ALIO YATENGENEZA KWA KITAMBAA CHA SANDA YAKADOLOLA AMNA ALIE YANUNUA ADI SASA HIVI WAKINA MAMA WA MADALE WAMEYAGEUZA KAMA NZINGA ZA KUBEBEA MAJI NA MATAMBALA YA KUMPIGIA DEKI ILA KINGKIBA TANGU ATOE TSHIRT ZAKE ZA KINGKIBA NA KOFIA NDO ZINAZONGOZA KWA KUUZA HII AFRICA NZIMA HADI JUZ JUZ WIZKIDAYO NA BLACKCOFEEE WALITUTUMIA ELA TUKAWATUMIA TSHIRT HIZO NA KOFIA ZA KINGKIBA KAMA MNABISHA NYIE WCB TEGEN MAT*KO YENU NA MSUBIRI TUTAWAPOSTIA PICHA ZAO MAT*KON MWENU SASA HUYU MAVUZI DOMO KAJA NA HIYO PERFYUM YAKE YA KIGANGA ILIO TENGENEZWA KWA MAJI YA MAITI BAADA YA KUONA KINGKIBA KAJA NA (IDCARD) ZA TEAMKIBA ET ILI DOMO AMKOMOE KIBA😈AKATI TANGU JUZI KADI ZA #TEAMKIBA ZITOKE TUMEISHA UZA CARD LAKI 5 AFRICA HII SASA WW #SUPERNYAMWERA HAYO MAPERFUM YAKO HUTOYAUZA YATADOROLA HADI MTAANZA KUMPULIZIA TIFA MATAK*N MWAKE KAMA PODA

Post hii iliufanya uongozi wa WCB ukose uvumilivu na kumkamata mhusika kiulaini kabisa.

“Kwa watu wote kama ulitukanwa na huyu ambae anaejiita @shilolekiuno_official kwa sasa yupo chini ya mikono ya sheria, Kama una mashitaka yoyote fika Oyster Bay Polisi, Vizuri ametaja watu wanaemtuma afanye hivyo! Na kuwasaidia wale ambao wanajiamini kuwa hawawezi kujulikana basi kwa taarifa yenu Serikali ina mkono mrefu sana! Eti Jana alikuwa anamuita Diamond “Simba”,” ameandika Sallam, meneja wa Diamond.

Dogo mwenyewe aliyekamatwa anatia huruma na haendani na uzito wa matusi aliyokuwa akiyaporomosha mtandaoni. Kalelewa kwa malezi gani mtoto huyu? Ni vijana wa aina gani tunao ndani ya paa za familia zetu ambao huishi kwenye kivuli cha majina bandia na kutukana watu matusi mazito!

Kijana huyu ni tone tu kwenye ndoa ya maji kwa idadi ya wengine waliojaa Instagram wakisubiri kutusi watu. Wapo wengi mno, wanawatukatana mastaa bila hata kosa na kuwapa wakati mgumu kwenye mtandao huo. Kukamatwa kwa @shilolekiuno_official ni mfano hai kuwa ni rahisi kuwakamata hata kama wamejificha nyuma ya majina bandia. Na hakika vijana wengi watajikuta kwenye matatizo makubwa kwa mchezo huu.

Wale ambao bado wanaendelea na mchezo huu watambue kuwa hali imeshabadilika na wanaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa kwa michezo wanayoifanya. Bahati mbaya wengi hawajui hatari ya wanachokifanya. Wakiwa wamejifungia kwenye vyumba vyao na kutumia majina bandia, wanadhani hakuna anayeweza kuwajua na kuwafikia. Hawajui kuwa wanachokifanya ni sawa na kuku aliyeficha kichwa chake kichakani asionwe, huku mwili mzima ukiwa nje.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM