Saturday, 19 November 2016

Kama wewe unapenda sana Selfie hii inakuhusu


 Kuna kausemi hapa mjini watu hupenda kukatumia kufikisha ujumbe kwa kina dada wapenda pesa ambao hawajui kuzitafuta kazi yao ni kupiga vibomu tu, utasikia wakiambiwa “kama unapenda pesa kaolewe na ATM Machine” lakini sasa kwa wale wanaopenda magari utadhani wamebatizwa na petroli hao ndio balaa kabisa. Kuna wengine wao selfie ndio kila kitu utafikiri walisoma photojournalism; yani kila mara popote alipo ni kujitwanga picha wee… na hivi siku hizi kuna powerbank ndio kabisaa hawahofii kwamba simu itazima.
 Sasa taarifa ikufikie wewe mpenda picha za selfie kwamba takwimu za utafiti uliofanyika hivi karibuni juu ya vifo vinavyochangiwa na upigaji picha vimekuwa vikiongezeka kila uchwao kwani mwaka 2014 walikufa watu 15, 2015 wakafariki watu 39 na mwaka huu kwa kipindi cha miezi nane ya awali tayari wamefariki watu 73.

Utafiti uliofanywa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Hemank Lambawa akishirikiana na wenzie wa Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon huko Pittsburgh umegundua njia ya kukabiliana na vifo hivyo ni kutengeneza App maalumu itakayokuwa ikitoa ishara mara mtumiaji awapo kwenye hatari ili aweze kujihami.
 Tazama baadhi ya picha ambazo watu wamekuwa wakipiga selfie licha ya kuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha.No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM