Wednesday, 30 November 2016

INASIKITISHA:ASKARI POLISI AFARIKI DUNIA KWA KUJIPIGA RISASI KWA BAHATI MBAYA

Tokeo la picha la SMG
ASKARI wa jeshi la Polisi mwenye cheo cha Koplo Evarist Furaha wa Kibaha Mkoa amefariki Dunia mara baaada ya kujifyetulia risasi kwa bahati mbaya akiwa kazini.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Blasius Chatanda ameyasema hayo jana kwa waandishi wa habari alipokuwa akitolea ufafanuzi tukio hilo.
Chatanda amesema ajali hiyo ilitokea Novemba 28, mwaka huu saa moja usiku, Maili Moja eneo la Sokoni, Kata ya Maili Mmoja.
“Askari huyo alijipiga risasi kwa bahati mbaya ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi,” amesema Chatanda.
Amesema, Furaha aliingia kazini jioni katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kibaha na alikuwa amepangiwa lindo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
“Alikutwa na mauti baada ya kujipiga risasi kwa bunduki aina ya SMG akiwa anakwenda kwenye lindo alilopangiwa,” amesema na kuongeza kuwa alikuwa anaenda lindoni akiwa amekaa mbele ya gari PT1732 lililokuwa likiendeshwa na Koplo Grayson, ndipo wakati anashuka bunduki ilijifyatua na kumpiga kifuani upande wa kushoto.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM