Saturday, November 12, 2016

Hili ndilo eneo ambalo mwili wa Samuel Sitta utapumzishwa


Baada ya viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam jana kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel John Sitta aliyefariki dunia November 7 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Mwili wa Samuel Sitta ulisafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi walipata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye ulisafirishwa kwenda Urambo Tabora ambako maziko yanatarajiwa kufanyika leo November 12 2016 majira ya saa nane mchana.
Kwenye hii video hapa chini ni eneo ambalo Mzee Sitta atazikwa, ni eneo la kuzikwa familia ya Sitta ambalo lipo  km 2 kutoka nyumbani kwake.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.