Sunday, November 13, 2016

Donald Trump “Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”“Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”, ni kauli ya Rais mteule Donald Trump baada ya kuulizwa kwamba atakuwa akiufanyia nini mshahara wa Dola laki nne (400,000 kwa mwaka) ambazo ni mshahara wa Rais wa Marekani anapokuwa Ikulu ya White House.
Kauli hii aliitoa Donald Trump mshindi wa kiti cha Urais nchini Marekani wakati akiwa kwenye kampeni zake September 17, 2015, huko Rochester, New Hampshire: “Kitu cha kwanza ninachotaka kuwaambia na nitakifanya kama nikichaguliwa kuwa Rais, Sitakuwa nikichukua mshahara, hata dola moja siihitaji, hicho sio kitu kikubwa kwangu.” – Donald Trump
Kwa mujibu ripoti mpya zilizotolewa na jarida la watu maarufu duniani Forbes, limetaja utajiri wa Rais huyo mteule kuwa unafikia Dola Bilioni 3.7 za Marekani ambazo ni zaidi ya shilingi Trilioni 8 za Tanzania
Katika Video hapa chini, Donald Trump anasikika akisema kwamba alikuwa akijigharamia kwa fedha yake mwenyewe wakati wa kampeni zake, hivyo hatachukua mshahara wake zaidi ya kupokea vitu vidogo ambavyo ni vya lazima akiwa Rais.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.