Tuesday, November 8, 2016

Diana Miss Tanzania alia na Kamati ya Miss Tanzania ‘zawadi sijapewa, sijafanyiwa maandalizi ya Miss World’

Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World’, ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza hali ambayo amedai inaweza kumfanya ashindwe kuiwakilista Tanzania katika mashindano hayo. dsc_0406
Mrembo huyo amedai bado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania na serikali, ikiwa zimebaki siku chache kuweza kufikia kwenye mashindano hayo ya dunia.
“Hata zawadi zangu zilizo haidiwa sijapewa, kwahiyo inakuwa ngumu kwangu kujiandaa na mashindano ya miss dunia,” Diana alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Siku ishirini zilizobaki ni ndogo natakiwa kuandaa documentary ya historia ya kimasai Arusha. Sina kitu chochote chakufanyia natakiwa nilipe hiyo, natakiwa nilipe team support kwa sababu natakiwa kwenda kuonyesha Tanzania yangu, natakiwa kuonyesha beauty of purpose,”
Aliongeza, “Tanzania, viongozi, serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve”
Kwa upande wa afisa uhusiano wa kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico amesema shughuli za maandalizi ya miss huyo zinafanywa na Kamati ya Miss Tanzania.
“Hayo mambo yanashughulikuwa na Kamati ya Miss Tanzania. Yaani ameshaanza kuongea na vyombo vya habari? Mimi sina mamlaka ya kulijibu hilo la zawadi lakini nachojua maandalizi yake yanafanyika na kamati,” alisema Rico.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.