Wednesday, 2 November 2016

Christian Bella: Sina shobo na collabo za kimataifa


King of Best Melodies CHRISTIAN BELLA amefunguka kuwa hana shobo na collabo za kimataifa.
13473283_548042955383857_1817904920_n
“Kuna idea ambazo nazifanyia process, lakini bado zijaanza process yoyote kuhusu collabo ya kimataifa. Na mimi kila siku huwaga sina haraka, najua kila kitu kina wakati wake na kama nikiamua kufanya collabo nitatangaza. Na sina presha pia ya collabo yoyote ya nje. Nachokuwa na presha nacho ni kutengeneza ngoma zinazokubalika nyumbani namaanisha Tanzania, East Africa kwa ujumla na Kongo,” amesikika Bella katika kipengele cha PIGIA MSTARI kinachosikika kupitia Kipindi cha THE SPLASH kinachorushwa na Ebony FM ya Iringa.
Katika hatua nyingine Christian Bella amezungumzia siri kubwa ya yeye kuwa na mashabiki wengi na ambao wanaongezeka kila siku.
“Kikubwa msanii unatakiwa kuwa mtu wa watu,” anasema. “Unatakiwa kuwa na discipline ya kazi. Pia unatakiwa kuwa mbunifu na mimi kinachonifanya niwe karibu na mashabiki wangu na kuongeza mashabiki wapya kila siku ni uwezo wangu wa kazi na kikubwa Mungu anampa kila mtu nyota kwahiyo hiyo nyota niliyopewa ina mchango mkubwa wa mimi kupendwa na watu,” ameeleza Bella.
Kuhusu Malaika Band, muimbaji huyo anasema, “Ujue Amerudi nimetoa mwaka jana. Unajua kitu ambacho kinawafelisha wasanii wa bendi nikuunganisha nyimbo ambazo hazifanyi vizuri lakini unaunganisha tu. Unajua kama umetoa wimbo wa bendi inabidi uiachie time ili ufanye vizuri. Wimbo kama amerudi bado una nafasi kubwa sana na bado mkubwa sana, sina haraka ya kutoa wimbo na bendi labda mwaka kesho, sisi hatufanyi mashindano.”
NA CHRIS BEE

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM