Wednesday, November 2, 2016

BONDIA THOMAS MASHALI AAGWA VIWANJA VYA LEADERS,AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI LEO

 Bondia Francis Miyeyusho, akilia kwa uchungu wakati akitoa heshima za mwisho kwa bondia mwenzake marehemu Thomas Mashali wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, mchana huu. 

Marehemu Mashali amezikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Pamoja na kukamilika kwa taratibu zote za maziko lakini bado shughuli hiyo ya msiba iligubikwa na utata kwa baadhi ya wanandugu na wadau wa mchezo wa ngumi kutokana na kutokamilika kwa maandalizi katika viwanja hivyo.

Aidha baadhi ya wadau wa ngumi walishikwa na butwaa na kubaki na sintofahamu kutokana na uwanjani hapo kutokuwepo Mchungaji wala Kiongozi yeyote wa dini kwa ajili ya kuendesha ibada ya maziko na kubaki na maswali mengi na hasa baada ya kuibuka utata wa kwamba marehemu kabla ya kifo chake alibadilisha dini na kuwa Muislamu na kuitwa Mohamed.

Hata hivyo Baba mzazi wa marehemu alipoulizwa kuhusu marehemu kubadili dini, kwa upande wake alisema kuwa yeye hatambui kuhusu mwanae kubadili dini na kwamba alishapanga kumzika kwa taratibu za Kikristo kama ilivyofanyika leo ambapo ibada ya maziko ilifanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Mwanasoka Athuman Chuji, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mashali wakati wa shughuli za kuaga mwili katika viwanja vya Leaders Club.
 Gari lenye mwili wa marehemu Mashali likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders.
 Ndugu, Jamaa na marefiki wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mashali lilipowasili kwenye Viwanja vya Leaders Club.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa Mashali wakiwa katika foleni
 Foleni ya kuaga mwili wa Mashali
 Bondia Francis Cheka akitoa heshima za mwisho mwili wa marehemu Mashali kwenye Viwanja vya Leaders Club.
 Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania TPBO, Yassin Ustaadh,akitoa heshima za mwisho.
 Bondia akitoa heshima za mwisho
 Dada wa marehemu akitoa heshima za mwisho
 Mdogo wa marehemu, Charles Mashali ambaye pia ni bondia, akitoa heshima za mwisho 
 Mke wa marehemu, Annastazia akitoa heshima za mwisho
Wajumbe wa Kamati ya maziko, akimsimamia mmoja kati ya waombolezaji aliyepiga picha ya mwili wa marehemu wakati wa kuaga. Wanakamati hao walitangaza kuzuia waombolezaji kupiga picha ya mwili wa marehemu

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.