Sunday, October 2, 2016

WATUMISHI WA SERIKALI WACHOMWA MOTO HADI KUFA WAKITUHUMIWA KUWA NI "WANYONYA DAMU" HUKO IRINGA MVUMI DODOMA

MNAMO TAREHE 01/10/2016 MAJIRA YA SAA 12:30 HUKO KIJIJI CHA IRINGA MVUMI KATA YA IRINGA MVUMI TARAFA YA MAKANG'WA WILAYA YA CHAMWINO MKOA WA DODOMA.

GARI NAMBA STJ 9570 AINA YA TOYOTA HILUX DOUBLE KEBEN MALI YA KITUO CHA UTAFITI WA UDONGO NA MAENDELEO YA ARDHI CHA SELIAN ARUSHA, LILICHOMWA MOTO NA WATU WALIOKUWEMO NDANI YA GARI HILO AKIWEMO DEREVA NA WATAFITI WAWILI MMOJA KATI YAO MWANAMKE, AMBAO MAJINA YAO HAYAJAJULIKANA WALIVAMIWA NA WANAKIJIJI CHA IRINGA MVUMI NA KUWAKATAKATA KWA MAPANGA,

PAMOJA NA SIRAHA ZA JADI KISHA KUWACHOMA MOTO HADI KUFA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI MWANAMKE MMOJA AITWAYE CECILIA D/o CHIMANGA, MIAKA 34, KUPIGA YOWE KIJIJINI KUWAFAHAMISHA KUASHIRIA KWAMBA AMEONA WATU AMBAO ANAWAHISI NI WANYONYA DAMU (MUMIANI),

TAARIFA HIZO ZILIPOFIKA KIJIJINI NDIPO MCHUNGAJI WA DHEHEBU LA CHRISTIAN FAMILY CHURCH AITWAYE PATRIC s/o MGONELA, MIAKA 46, MGOGO MKAZI WA KIJIJI CHA IRINGA MVUMI, AMBAYE ALIKITANGAZIA KIJIJI KUPITIA KIPAZA SAUTI CHA KANISANI KUWA WAMEVAMIWA NA WANYONYA DAMU (MUMIANI) NDIPO WANAKIJIJI WAKAENDA KUCHOMA GARI NA KUWAUA NA KUWACHOMA MOTO.

BAADA YA TUKIO HILO, MSAKO UKIJUMUISHA ASKARI WA KAWAIDA, MAKACHERO NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU) WAKIWEMO MAOFISA WANNE, ACP ERNEST KIMOLA, SO1 DODOMA, SSP MOHAMED KILONZO RCO DODOMA, ASP OSCAR FELICIAN OC FFU DODOMA NA ASP MAULID MANU OC CID (W) CHAMWINO,
WAKAGUZI WAWILI, NA SECTION TATU ZA R&F, MIILI YA MAREHEMU HAO IMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA MISSION MVUMI, MSAKO UNAENDELEA. 
Credit to Malunde1 Blog
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.