Thursday, October 6, 2016

Ukinunua Iphone 7 nchini China huna kazi!


Kampuni kadhaa nchini China zimetangaza kuwafuta kazi wafanyakazi wake watakaoingia madukani kununua simu mpya za kampuni ya Apple ambazo ni Iphone 7.
iphone7s
Baadhi ya kampuni hizo zimedai kuwa zimeamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na sababu za kizalendo huku nyingine zikisema zinataka kuwafundisha wafanyakazi wake kutopenda sana raha na anasa za dunia.
Mtandao mmoja umemnukuu msemaji wa kampuni ya Nanyang Yongkang Medicine, Liu akisema lengo la agizo hilo ni kuwahamasisha pia wafanyakazi kuangalia zaidi familia na kuachana na vitu vya starehe ambavyo si vya lazima.
Hata hivyo baadhi ya watu wamesema kuwa maamuzi ya makampuni hayo huenda kukawadhuru wachina wenyewe kwa kuwa uzalishaji wa simu za Apple hufanywa katika viwanda vya kampuni ya Foxconn nchini Uchina.
Simu hizo zinauzwa kwa kiasi cha $1,047 kwa nchi ya China.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.