Sunday, 2 October 2016

Simba na Yanga zapigwa marufuku na serikali kuutumia uwanja wa Taifa

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ametembelea Uwanja taifa Jumapili hii na kuzipiga marufuku mechi zote za Yanga na Simba kufanyikia uwanjani hapo kutokana na uharibifu wa mageti na viti uliojitokeza siku ya jana katika mechi hiyo ya watani hao wa jadi. mabomu-ya-machozi Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi hapo jana baada ya kufanya uharibufu wa viti
Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.
“Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu,” alisema Nape. alisema Nape.
Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM