Thursday, October 6, 2016

SERIKALI YAMVUA MADARAKA MKUU WA SHULE YA MBEYA DAY KWA KUFUMBIA MACHO UKATILI DHIDI YA MWANAFUNZISerikali ya Tanzania imeagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kanda ya video ilioonyesha kundi moja la walimu likimpiga mwanafunzi.


Mwalimu mkuu wa shule hiyo tayari amesimamishwa kazi kwa mda kwa kutochukua hatua hata baada ya kugundua kuhusu kisa hicho ,taarifa ya serikali imesema.

Raia wa Tanzania katika mitandao ya kijamii walionyesha hasira zao ,wakiitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya washambuliaji hao.

Video hiyo ambayo haijakaguliwa inaonyesha mwanafunzi mmoja akipigwa na kundi la walimu katika kile kinachoonekana kuwa chumba cha wafanya kazi wa shule.

Katika kanda hiyo ya sekunde 38,takriban watu watano wanaonekana wakikabiliana na kushambulia mvulana huyo aliyeanguka chini kwa kumpiga ngumi pamoja na mateke.

Adhabu ya kupigwa viboko ni haramu nchini Tanzania,na kisa hicho cha hivi karibuni kinatarajiwa kuzua mjadala kuhusu utekelezwaji wa sheria hiyo katika shule za taifa hilo.


ANGALIA HAPA VIDEO YA MWANAFUNZI ALIYEPEWA KIPIGO NA WALIMU AKISIMULIA MKASA HUO
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.