Monday, October 3, 2016

RAIS MAGUFULI : HAKUNA FEDHA ZA TETEMEKO KWENDA MAGEREZA,WAFUNGWA WATETEMEKE KUJENGA MAGEREZA YAOImage result for rais magufuli“Katibu Mkuu Kiongozi, hakuna kuwapelekea wafungwa wa Karagwe fedha yoyote, hizi za maafa ya tetemeko. Watetemeke na kufanya kazi,” alisema Rais Magufuli na kuibua kicheko kwa watu waliohudhuria hafla hiyo.
Rais John Magufuli amesema Serikali haitajenga Gereza la Kitengule Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera lililobomoka kwa tetemeko la ardhi, badala yake ameliagiza Jeshi la Magereza liwatumie wafungwa kufanya kazi hiyo.
Alitoa agizo hilo juzi wakati akifunga mazoezi ya kijeshi ambayo kitaalamu yanaitwa ‘amphibious landing’ yaliyofanyika Kijiji cha Baatini, Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Katika mazoezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kushuhudia wanajeshi wakilikomboa eneo lililotekwa na maadui ukanda wa majini, Rais Magufuli alimtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kutopeleka fedha za maafa kujenga gereza hilo
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.