Saturday, October 22, 2016

Prof Ndalichako aiagiza Bodi ya Mikopo kurudisha mfumo wa zamani wa utoaji mikopo

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wakutoa fedha kwa wanafunzi wa chuo. necta
Akizungumza katika mahojiano maalum Alhamisi hii katika runinga ya TBC Taifa, Waziri Ndalichako alikiri kutokea mapungufu katika mchakato wa ugawaji wa mikopo.
“Kama waziri nimeshaiagiza Bodi ya Mikopo kwamba kwa sababu wanafunzi tayari wapo mashuleni, warudi katika utaratibu ule huwa wanawapa, kwa maana kwamba wanaangalia uhitaji ili mtu ambaye anastahili kupata apatiwe fedha bila kufanya makosa kwenye chakula angalau kwa muhula wa kwanza. Halafu kama kutakuwa kuna haja yakufanya kulingana na uwezo, vile vigezo viwekwe wazi na wanafunzi waelimishwe lakini lengo letu lipo pale pale kwamba wanafunzi wenye uhitaji watapatiwa mkopo,”
Waziri huyo alisema Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu imelazimika kubadili mfumo wa utoaji mikopo ili kukabiliana na mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku wachache wakipewa kiasi kidogo ambacho kinadaiwa hakitoshelezi.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.