Tuesday, 4 October 2016

PICHA:TASWIRA SOKO KUU LA MORO BAADA YA KUVUNJWA

 Soko hili lilijengwa mwa
ka 1953.
 Kufuatia Mto Kikundi kukatiza jirani na Soko hilo, Msimu wa masika mto huo hufulika na majiya hujaa katikati ya Soko hilo na kusababisha adha kubwa kwa wafanyabiashara na wateja wa Soko hilo.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
BAADA ya Mvutano wa Muda mrefu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na wafanyabiashara wa Soko Mkuu hatima juzi Soko hilo limevunjwa kwa lengo la kupisha ujenzi wa Soko la kisasa.
Awali wafanyabiashara hao walicha ya kupewa Notisi waligoma kuondoka kwenye Soko hilo wakitaka kuhakikishiwa mambo mawili Mosi Kupelekwa eneo lingine la kufanyia biashra kupisha ujenzi huo Pili kuhakikishiwa kurejea pindi Sko hilo jipya litakapo kamilika.
Akizungumza na Mtandao huu Mmoja waviongozi wa Soko hilo Jihihada Kidogo Maarufu kwa Jina la Kitonsa alisema.
" Kimsingi hakuna Mtu anayekataa maendeleo kwetu sisi ujeni wa soko jipya ni faraja kwetu kwani wakati wa Maskika adha tunayoipta sisi na wateja wetu ni Mkubwa sana.
Utata ni kwamba tunataka Mikababa ya sisi kurejea pindi Soko litakapo kamilika pia tunataka Manispaa watutafutie eneo katikatika ya Mji la sisi kufanya biashara wasitupeleka nje ya mji ambako baadhi ya wateja wetu wataashindwa kufika mfano Mzungu hawezi kwenda Soko la Mji Mpya au Mazimbu hivyo ili tusipoteze wateja wetu watutafutie eneo la katikatika ya Mji"alisema Kitonsa ambaye ni Mkazi wa Mji Mpya.
Kwa sasa wafanyabiashara hao wamehamishiwa Manzese ambapo kblabu cha Pombe za Kienyeji cha Manzese kimevunjwa na kujengwa Soko hilo la Muda. 
 
chanzo:shekidele blog

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM