
Mchekeshaji wa bongo movie Mboto Haji ameamua kumuombea msamaha Tunda
Man kwa kudanganya kumtumia kwenye filamu, Mama Kijacho ambayo
haijawahi kufanyika.

Tundaman alidai kuwa wapo kambini wakiandaa filamu hiyo ambayo ni
jina la wimbo wake. Kwenye video yake wameonekana Mboto na Riyama.
Akiongea na E-News, Mboto alisema, “Nawaomba mashabiki wa Bongo Flava
na bongo movie kumsamehe Tunda Man kwa kauli yake hiyo aliyoitamka
ambayo haikuwa na ukweli ndani yake. Hata mimi nimeshamsamehe kwa moyo
safi kabisa.”
No comments:
Post a Comment