Wednesday, 5 October 2016

Kuvamiwa kwa Kim Kardashian ni kiki? Wapo wanaoamini hivyo

Maswali mengi yameibuka wiki hii baada ya taarifa za kuvamiwa kwa Kim Kardashian na majambazi waliovaa mavazi ya polisi mjini Paris na kuiba vitu vyenye thamani ya dola milioni 10, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 21.
kim1
Baadhi ya vyombo vingi vya habari vimekuwa vikipinga ripoti hiyo kwa kudai kuwa ni kiki ya kibiashara. Moja ya vyombo hivyo vinavyoonekana kutoziafiki taarifa hizo ni gazeti la Daily Mail la Uingereza kwa kuandika maswali juu ya tukio hilo na uhalisia wake.
Haya ni maswali ya gazeti hilo yanayoonyesha kuwa tukio hilo linaweza likawa ni lakutengeneza.
1.Kwa nini Kim na rafiki yake kipenzi, Simone Harouche walibaki chumbani wenyewe bila mlinzi wakati wakijua wana vito vyenye thamani kubwa na kujipiga picha kwenye mitandao ya kijamii?
2.Kwa nini hakukuwa na kamera za CCTV katika nyumba hiyo ambayo ni ya gharama kubwa. Nyumba hiyo inalipiwa karibu shilingi milioni 60 kwa wiki.
3.Kwanini awepo mlinzi mmoja tu kulinda hoteli hiyo ya gharama ambayo nyota wakubwa kama Madonna na Leonardo Di Caprio hupanga? Nyumba hizo zina mpishi maalum, dereva na watumishi wengine.
4.Majambazi waliwezaje kuingia kwenye mlango wa hoteli hiyo wakati unalindwa na mitambo maalum? Milango haikuonyesha kama mtu alilazimisha kufungua au kuvunja kitasa.
5.Ni taarifa gani mlinzi aliyekuwepo lindo siku hiyo alikuwa nazo kuhusu Kim na wenzake hadi alipobanwa na kufungwa na majambazi akazitoa?
6.Kwa nini mlinzi wa Kim Pascal Duvier aliondoka na kumuacha mwanamitindo huyo peke yake. Majambazi walijuaje kuwa Kim yupo peke yake?
7.Kwa nini Kim aliruhusiwa kuondoka Ufaransa saa chache baada ya kuvamiwa?

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM