Tuesday, 4 October 2016

Kim Kardashian asimulia alivyovamiwa Paris ‘nilidhani watanibaka, niliomba wasiniue sababu nina watoto’

Kim Kardashian amesimulia tukio la kuvamiwa jijini Paris, Ufaransa – na hakika lingeweza kukatisha maisha yake.
kim1
Anasema aliamrishwa aondoke kitandani na watu waliokuwa wamefunika sura zao ambao awali alihisi walikuwa wanataka kumbaka. Vyanzo vimeiambia TMZ kuwa alikuwa amelala kitandani na nguo ya kulalia aliposikia mlio wa viatu vikipanda ghorofa katika nyumba hiyo yenye ghorofa mbili.
Wanasema Kim aliona walau mtu mmoja aliyekuwa akiwa amejifunika uso na mwingine akiwa amevalia kofia ya polisi kupitia dirisha la vioo. Alijua tu kuwa kuna kitu hakikuwa sawa, hivyo aliondoka kitandani na kujaribu kumpigia simu bodyguard wake.
3912732300000578-0-image-a-1_1475532331805
Kabla hajamaliza kupiga, mmoja kati ya watu hao alimpokonya simu mkononi mwake. Walimfunga mikono yake na pingu za plastiki na kumzungushia ‘sole tape’ mwili mzima. Wanasema mmoja alimshika kwenye kifundo cha mguu. Kim aliwaambia polisi kuwa hapo ndipo alipodhani wangembaka.
Walimwekea tena sole tape kwenye vifundo vyake vya mguu, walimnyanyua na kumweka bafuni. Alianza kupiga kelele, akiwaomba wasimuue sababu alikuwa na watoto. Aliwaambia kuwa alikuwa na hela na kwamba wachukue chochote wanachotaka.
Kim aliwaambia polisi kuwa majambazi hao walikuwa hawajui Kiingereza na walizungumza Kifaransa tu. Kitu kimoja anasema alielewa, watu hao walikuwa wakisema, “ring, ring.” Kim alijua kuwa walikuwa wanaitaka pete aliyopewa na Kanye – yenye thamani dola milioni 4. Aliwaambia kuwa ilikuwemo ndani ya nyumba hiyo, lakini huo haukuwa mwisho.
Kim aliendelea kuomba na kulia, na hapo ndipo jamaa hao walipoamua kumziba mdomo kwa tape kumnyamazisha. Vyanzo vinasema rafiki wa Kim, Simone naye alikuwa ndani ya mjengo huo, kalala kwenye chumba ghorofa ya chini. Simone alisikia varangati hilo, alijifungia bafuni na kumpigia, Pascal, bodyguard wake ambaye wakati huo alikuwa na dada yake, Kourtney … kuwaeleza kuwa waende haraka sababu kulikuwa na kitu cha hatari kikiendelea.
Pascal alifika hapo dakika 2 baada ya majambazi hao kuwa wameondoka. Tukio zima lilichukua takriban dakika 6 tu. Majambazi hao walichukua mikufu, pete, simu, credit cards na vitu vingine vinavyofikia thamani ya dola milioni 10.
Polisi wa Ufaransa wanahisi kuwa tukio huenda likawa limepangwa na mtu wa ndani wa timu ya ulinzi ya Kim aliyewapa ramani yote.
Chini ni picha ya nyumba hiyo aliyokuwa amefikia Kim Kardashian.
161003-kim-kardashian-paris-01
161003-kim-kardashian-paris-02
161003-kim-kardashian-paris-03
161003-kim-kardashian-paris-04
161003-kim-kardashian-paris-05
161003-kim-kardashian-paris-07


No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM