Saturday, October 22, 2016

Kichuya huenda akatua klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini

Mchezaji wa klabu ya Simba ambaye hadi saivi ameonyesha kiwango cha juu tangu asajiliwe na Simba winga Shiza Kichuya huenda akaihama timu hiyo na kutua Chippa United ya Afrika Kusini baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kuvutiwa naye.
shiza-kichuya-simba-2016_12v0abroioot81smmfxzi3nc9e
Wakala wa kusaka wachezaji wa timu ya Chippa, Rodgers Mathaba ameuambia mtandao wa Goal, kuwa wamevutiwa na mchezaji huyo baada ya kumfatilia katika baadhi ya mechi alizoichezea timu yake ya Simba na anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo.
“Tumevutiwa na kipaji cha Kichuya na tupo tayari kumnunua endapo tutafikia muafaka na klabu yake anayoichezea ya Simba,” amesema Mathaba.
Itakuwa ni neema kwa klabu ya Simba na Kichuya mwenye ambaye ametua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar na amekuwa na mwanzo mzuri hadi kufikia hapo alipo.BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.