Wednesday, October 5, 2016

Bodi ya Wadhamini yawaendea Mahakamani Profesa Lipumba, Msajili

Leo October 5, 2016 nimeipata stori hii kutoka Bodi ya udhamini ya chama cha wananchi CUF kuhusu kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya msajili wa vyama vya siasa nchini pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba kwa madai ya kuingilia mamlaka ya chama hicho.
Taarifa ya Wakili Nassor Juma imesema kuwa bodi ya udhamini ya CUF imefungua shauri hilo ikitaka kupata amri ya mahakama ili kumzuia msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kufanya shughuli za kisiasa nje ya mamlaka aliyopewa na sheria na kanuni za vyama.
Na kwa mujibu wa Wakili huyo amesema shauri hilo limefunguliwa na Bodi ya wadhamini ambao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho kuhusu chama.
>>>>Shauri limefunguliwa na bodi ya wadhamini wa chama dhidi ya msajiili wa vyama, Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi wengine 12. Bodi ya wadhamini wa chama cha wananchi CUF ni moja tu hivyo msajili hana bodi ya wadhamini tofauti hii ambayo imesajiliwa kwake hivyo walioleta shauri hili mahakamani ni bodi ambao ndiyo wenye mamlaka:- Wakili Nassor


0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.