Friday, 30 September 2016

WEMA SEPETU ATOA SABABU KUTOFANYA BIRTHDAY PARTY MWAKA HUU


Jana September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Tz Sweetheart Wema Sepetu, kama ilivyozoeleka katika siku ya kuzaliwa ya mwanadada huyo huwa party ya kujipongeza inahusika lakini mwaka huu imekuwa tofauti.
Wema Sepetu amefunguka kuwa hawezi kufanya party kwa mwaka huu na mwaka ujao na hivyo anajipanga kufanya bonge la party mwaka 2018 ambapo atakuwa anatimiza umri wa miaka 30.
Mwaka jana tulishuhudia mwanadada huyo akijizawadia gari aina ya Range Rover kama kujipongeza katika kusherehekea siku yake hiyo ya kuzaliwa, hatujui mwaka 2018 kipi kitatokea maana amedai kufanya bonge la party.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM