Thursday, September 29, 2016

WATUMISHI 3 WA SERIKALI NA MENEJA WA BENKI YA CRDB TAWI LA BUKOBA WAMEPANDISHWA KIZIMBANI


WATUMISHI watatu wa serekali akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016.
Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo leo ni aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Amantus Msole,mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin Makonda,Muhasibu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa banki yaCRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa.

Akiwasomea mashtaka yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Bukoba wakili wa serekali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni watuhumiwa walikula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye no.015225617300 ,ambapo wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba no.0150225617300
Alilitaja shitaka la pili kuwa ni watuhumiwa wanashitakiwa kwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.
Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana wateja wao kwakuwa bado ni watumishi wa serekali na wanao uwezo wa kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera
Hakimu Mkazi wa mahakama ya Bukoba Denis Mbelemwa alihairisha kesho hiyo hadi kesho saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na kujiridhisha kama watuhumiwa wanasitahili dhamana na kutaka watuhumiwa warudishwe rumande.
"Nahairisha shauri hili hadi kesho asubuhi saa tatu nikapitie tena vifungu vya sheria,kutokana na ukubwa wa kesi hii nione kama watuhumiwa wanadhaminika"alisema

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.