Monday, 26 September 2016

Wasanii wa bongofleva waibuka washindi katika mechi ya kuchangia waathirika wa tetemeko Kagera

Wasanii wa muziki wa bongofleva wameibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya wasanii wa bongomovie katika mechi ya hisani kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba. bongofleva-wakishangilia-ushindi Wasanii wa bongofleva wakishangia ubingwa wao
Mechi hiyo ilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya moja moja, magoli yaliyopatika katika kipindi cha kwanza. Goli la wasanii wa bongo movie lilifungwa na Mteze na dakika chache baadae H.Baba aliweza kuisawazishia timu yake kwa goli la kichwa.
Katika mechi nyingine kati ya wabunge wa Yanga na wabunge wa Simba, wabunge wa Yanga waliondoka na ushindi baada ya kuwafunga wabunge wa Simba goli 5 kwa 2. Angalia picha za matukio mbalimbali.
nape-akisalimiana-na-young-killer-msodoki Young Killer akisalimiana na Waziri, Nape

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM