Saturday, 17 September 2016

Uhakiki wa vyeti kwa watumishi kuandaliwa katika vituo maalum

Serikali imesema imeendelea na zoezi la kuhakiki vyeti vya utumishi ingawa suala hilo limeendelea kuleta usumbufu.
2110-1
Akiongea Ijumaa hii wakati akiahirisha bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliagiza kuwepo na vituo maalum ili kuharakisha zoezi hizo.
“Serikali imeendelea na zoezi la kuhakiki vyeti vya utumishi, ingawa limeendelea kuleta usumbufu kwa watumishi katika baadhi ya maeneo, naagiza kwa wakurugenzi kuandaa vituo maalumu kwa zoezi hilo vilivyo jirani na vituo hivyo vya wafanyakazi,” alisema Majaliwa.
“Badala ya kuwakusanya watumishi hao eneo moja, ni jambo ambalo linaleta usumbufu, ili kupunguza adha na gharama, halmashauri zote zizingatie agizo hili kwamba maafisa utumishi waende kwenye maeneo ya watumishi hawa kupanga vituo,”aliongeza.
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM