Thursday, 1 September 2016

TAZAMA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA LEO HUKO RUJEWA MKOANI MBEYA LEO,RC WA MBEYA NA SONGWE WAONGOZA WANANCHI KUSHUHUDIA TUKIO HILO

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) , Pascal Shelutete wakiangalia tukio la kupatwa kwa Jua kutumia vifaa maalum muda huu, katika eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya. Tukio hilo limeonekana vizuri zaidi katika eneo hilo kuliko maeneo mengine nchini. Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia wako katika eneo hilo, kushuhudia kwa uzuri tukio la kupatwa kwa Jua.
Hivi ndiyo jua lilivyoanza kuonekana baada ya kupatwa, Hapo ni eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya, eneo lililotengwa kwa ajili ya kutizamia tukio hilo kwa uzuri zaidi.
 
Na hata kina sie huku Mjini Dar es salaam tumelishuhudia tukio, japo tulitandwa na wingu zito. ila si haba tumebahatika kuiona kwa namna hii.
 
 Baadhi ya wananchi wakiendelea kushuhudia kupatwa kwa jua 
 Muonekano wa kupatwa kwa jua huko Rujewa leo
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amoss Makala akizungumza na wakazi wamji wa Rujewa waliojitokeza kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua mkoani Mbeya
 Jua jinsi linavyoonekana kwa kutumia karatasi maalumu ambayo unaweza kuona jua katika mandhari mbalimbali.
 Kikundi cha ngoma wakitumbuiza katika eneo ambapo kupatwa kwa jua kumetokea na kuonekana kwa kutumia kifaa maalumu Rujewa Mkoani Mbeya.
Biashara zikiendela katika eneo la Rujewa Mkoani Mbeya kama ijulikanavyo Mkoa wa Mbeya kwa Kulima Mpunga hapo biashara ya Mchele ikiendelea.
Mamalishe nao hawakusita kuona fursa iliyojitokeza katika eneo Lujewa Mkoani Mbeya kuhudumia wananchi wanaoenda kutazama kupatwa kwa jua.
Mwananchi akijiandaa kuangalia jua kwa kutumia karatasi maalumu.
Picha na Fadhili Atick na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM