Thursday, 8 September 2016

Show za Mr Blue Fiesta Wengi Wadai Ndio Msanii Bora wa Tanzania Kwa Sasa.....

Kwa mujibu wa Mrisho Mpoto, Harry Sameer, wamjua zaidi kama Mr Blue, anastahili kuwa msanii bora Tanzania.

Mpoto alidiriki kusema hivyo baada ya kushuhudia show ya hitmaker huyo wa ‘Mboga Saba’ akitumbuiza kwenye Fiesta mjini Shinyanga na kudai kuwa hajawahi kuona show moto kama ile.

“Naomba leo niseme kwa mara ya kwanza kwamba Mr Blue anastahili kuwa msanii bora katika nchi yetu ya Tanzania,” alisema Mpoto kwenye promo ya show hiyo iliyoruka Clouds FM.

Kwa miaka mingi Mr Blue amekuwa akisifiwa kwa uwezo mkubwa wa kutumbuiza jukwaani. Mwaka juzi wakati wa show hiyo pia, Kabayser alitajwa na waandaji wa Fiesta kuwa msanii aliyepata shangwe kuliko wote. Kipindi hicho alikuwa akihit na wimbo wake Pesa.

Kwa sasa Blue anafanya vizuri na wimbo wake ‘Mboga Saba’ aliomshirikisha Alikiba.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM