Saturday, September 17, 2016

Shilole Aeleza Kilichomsukuma Kupatana na Nuh Mziwanda

Baada ya hivi karibuni Sholole na Nuh Mziwanda kupatana, Shilole amefunguka na kuzungumzia nini kimemsukuma mpaka akapatana na mkali huyo wa wimbo ‘Jike Shupa’.
Wawili hao ambao walikuwa wapenzi waliachana kwa kutupiana maneno huku Nuh Mziwanda akionekana kumlaumu Shilole kwa kumpotezea muda.

Akiongea na Uhead ya Clouds FM Ijumaa hii, Shilole amedai ameamua kumaliza tofauti zake na Nuh Mziwanda kwa kuwa muimbaji huyo wa ‘Jike Shupa’ alikuwa anapoteza kujiamini pale anapokutana naye.

“Nikwambia kitu situation moja ambayo ipo, Nuh akiniona mimi huwa anapoteza kujiamini,” alisema Shilole. “Sasa ili kumueka sawa na aweze kuwa vizuri lazima na mimi nimwonesha am good. Kwa hiyo alivyoniona nipo good na yeye akawa fresh na furaha imerudi na nazani maisha yanaendelea,”

Hata hivyo mkali huyo wa wimbo ‘Say My Name’ alikanusha kurudiana na Nuh Mziwanda huku akidai kwa sasa wao ni washkaji.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.