Saturday, 10 September 2016

Ruby amjibu Diva baada ya kudai kuwa hamfahamu

 http://assets.audiomack.com/omary-ramsey/ccdbb1c1400545bd3da658def9024e77.jpeg
Ruby amefunguka na kusema kuwa kauli aliyoitoa mtangazaji huyo anaiona ni kama utoto. “Naona ni ujinga, I don’t want to talk about it, naona ni utoto sidhani kama ninaweza kuliongelea hilo.”
“Everybody knows me, so nahisi huo ni utoto tu labda wa kukosa majibu kwenye maswali ya interview aliyohojiwa. I don’t to talk about her,” ameongeza.
Pia Ruby amedai kuwa licha ya kuzinguana na uongozi wa THT, bado mambo yanaenda mswano.
“Kutokuwa na mawasiliano mazuri na uongozi wangu wa zamani sijaathirika kwakweli, sitaki kuliongelea hilo kwa sababu mimi naona kwangu ni kitu ambacho kimeshapita nataka niongelee vitu ambavyo vinaendelea mbele. Sidhani kama nina tofauti na wao mimi sijui ila, I don’t talk about them, at all.”
Inawezekana Diva alitoa kauli hiyo kutokana na Ruby kutokuwa na mawasiliano mazuri na Clouds Media baada ya kushindwa kuhudhuria kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika Mwanza, August 20 ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM