Monday, 5 September 2016

RAYMOND NA SNURA MAPYA YAIBUKABAADAYA PICHA HIZI KUVUJA


Staa wa Ngoma ya Chura, Snura Mushi, juzikati alieleza jinsi anavyowewesekea penzi la mwanaume ambaye ni staa mwenzake wa Bongo Fleva lakini hakumtaja. Katika pekuapekua, Wikienda limenyaka jina la staa huyo kutoka kwa mtu wa karibu wa Snura ambaye amedai kuwa ni Raymond au Rayvanny wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).
 Sosi huyo ambaye hakutaka kuchorwa gazetini alidai kuwa, Snura amekuwa karibu na Raymond na ukaribu wao ulizidi baada ya kufanya video ya msanii huyo ya Natafuta Kiki ambapo ndani yake walionesha mambo yao ya chumbani kama mapichapicha yanavyoonesha mitandaoni. “Kama mnakumbuka Snura alitangaza kuwa kati ya majina matano ya wanaume maarufu wa muziki Bongo, yupo mmoja anayemuwewesekea, jina la Raymond lilikiwemo.

“Baada ya video ya Natafuta Kiki, mapichapicha yalianza kumwagwa lakini unaambiwa kuna picha nyingine ambazo haziwezi kuwekwa gazitini kwani ni balaa na kwenye video picha hizo hakuna,” alitonya mnyetishaji huyo. 

Baada ya ubuyu huo kumwagwa juu ya meza ya Wikienda , wanahabari wetu walitinga nyumbani kwa Snura kisha kumuweka mtukati juu ya sakata hilo ambapo mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo; Wikienda:  Snura, picha zako na Raymond zinakuonesha ukijiachia bila masihara, je, kuna nini kinaendelea au nako ni kutafuta kiki? Snura: Hahahaaa… niliamua kufanya kweli kwani mtu anapokupa kazi yake lazima uitendee haki. Kwani kuna ubaya gani? Wikienda: Inasemekana Raymond ndiye yule ambaye wiki kadhaa zilizopita ulisema anakukosesha usingizi na unampenda ndiyo maana hata mabusu yenu ni zaidi ya video na kuna kitu kinaendelea kati yenu, je, nini kinaendelea? Snura:  Mh! Watu wataongea mengi kweli ila ipo siku watamjua ninayemzimikia. Kama ni Raymond nitasema. 

Kwa sasa mimi na Raymond tumefanya video na sijaona la kushangaza. Wikienda: Je, kwa pozi lile mpenzi wako uliyenaye hajakasirika? Snura: Mpenzi? Yupi tena? Mimi niliamua kufanya kweli hakuna wa kuniuliza. Watu wanashangaa pozi hilo? Mbona zipo picha kali kabisa ambazo hata kwenye video hakuna? Sikuona la kushangaza hapo na hakuna wa kunizuia mimi kufanya mambo yangu. Wikienda: Lini utamuweka wazi umpendaye? Snura: Naanza kumuweka wazi hivi karubuni. Nitaanza na mkono, baadaye kiungo kimoja baada ya kingine, mwisho mtamuona, hahahahaa watu wana hamu eee… mbona watamjua tu! Wikienda: Lakini wewe na Raymond inasemekana mna mawasiliano ya ziada kama wapenzi kwani hata picha nyingine mbali na video zinawaonesha mkiwa pamoja, unalizungumziaje hilo? Snura: Mnachimba sana ila ipo siku mtaujua ukweli. Sipendi kutangaza uhusiano mara kwa mara maana mwisho naonekana sifai wakati ninaoingia nao kwenye uhusiano ndiyo hunisaliti na kunishinda. Ila kwa huyu anayekuja, inshallah penzi ni kikohozi kulificha huwezi, kama ni yeye (Raymond) basi mtaujua ukweli. 


RAYMOND VIPI? Baada ya Snura kufunguka hayo, mwandishi alimwendea hewani Raymond lakini hakupatikana kwa maelezo kuwa yupo nchini Kenya. Alipotumiwa chatting na Wikienda kupitia WhatsApp kuulizwa ishu hiyo alijibu kwa kifupi: “Jamani nooo…hahaha…ile ni kazi tu, ilibidi tuvae uhusika but nothing else (lakini hakuna kingine chochote).

” NI MWENDELEZO? Kumekuwa na kasumba ya mastaa wa kike wenye umri mkubwa kutoka kimapenzi na vijana wadogo kiumri hivyo wapenda ubuyu wananyetisha kuwa inawezekana Snura anaendeleza kasumba hiyo baada ya Jacqueline Wolper, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Wema Isaac Sepetu na wengine.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM